Akaunti za mitandao ya kijamii za klabu ya Barcelona zadukuliwa

Akaunti za mitandao ya kijamii za klabu ya Barcelona ya Hispania jana usiku zimeduliwa na watu wanaosadikika kuwa ni watu wa karibu klabu hiyo


Mapema kuamkia leo alfajiri Akaunti zao za Twitter na Facebook zilianza kuposti picha na habari za kumkaribisha winga wa kulia wa klabu ya PSG, Ángel Di María kitu ambacho kiliwashangaza mashabiki wa Barcelona mitandaoni.
Wadukuzi hao walionekana ni watu wa karibu kwani walijitambulisha huku wakihitaji mawasiliano na klabu hiyo ili waweze kurejesha kurasa hizo.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kukumbwa na udukuzi kwani mwaka 2014 walikubwa na tatizo hilo ambapo wadukuzi walishinikiza klabu hiyo iachane na udhamini na kampuni ya Qatar Airways .
Barca-twitter-1.jpg