Anachotamani Young Killer kirejee katika Bongo Flava

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Young Killer amesema anatamani yarejee mashindano ya Mkali wa Rhymes.



Rapper huyo ameeleza kuwa mashindano hayo yalileta changamoto katika muziki hasa wa rap na kufanya wasanii kutoa kazi nzuri zaidi.
“Mkali wa rhymes ni mashindano ambayo yalikuwa yanaleta chachu kila mtu anakuwa anakaza kwa sababu wanajua dakika za mwisho kutakuwa na mashindano na mshindi anabidi apatikane, so kama una kazi mbaya inamaana hautoshinda, so kulikuwa kuna mlazimu mtu aweze kukaza,” ameiambia Dj Show ya Radio One na kuongeza.
“Ukiangalia hata katika tuzo category ya hip hop ndio huwa ya mwisho kwa sababu inakuwa na changamoto ndio watu huwa wanaisubiria kwa hamu, so inafanya hata utamaduni wetu wa rap/hip hop unakuwa unazidi kusogea mbele, hivyo natamani hayo mashindano yakirejea,” amesema Young Killer.
Mwaka 2012 Young Killer alishinda katika mashindano ya Super Nyota chini ya Clouds Media Group na ikawa mwanzo wa yeye kuanza kushika chart katika Bongo Flava.
By Peter Akaro