Staa wa filamu za James Bond akubali kurudi kwa mara ya mwisho

Unatamani kumuona tena Daniel Craig kwenye kwenye filamu za James Bond? Basi kaa tayari kwa ujio huo.



Akiongea katika kipindi cha runinga cha The Late Show with Stephen Colbert, muigizaji huyo ambaye ni raia wa Uingereza amethibitisha kuwa ataigiza katika filamu hiyo mpya ya 007 kama James Bond inayotayarishwa na kampuni ya MGM.


“Ndio. Tumekuwa tukilijadili, tumekuwa tukijaribu kukubaliana jinsi mambo yataenda. Nimekuwa kwa muda mrefu nikitaka kupumzika. Ninataka kuondoka nikiwa bado navuma, nasubiri kwa hamu sana,” amesema Craig katika kipindi hicho.
Filamu hiyo mpya ya James Bond ambayo inatarajiwa kuwa ya 25, inadaiwa kuachiwa Novemba 2019. Mwezi Mei mwaka jana Craig alidaiwa kukataa ofa ya £68 kutoka katika kampuni ya MGM ili acheze filamu hiyo na baadae Tom Hiddleston alitajwa ndiye anategemewa kuwa James Bond mpya.
Mpaka sasa Daniel Craig ameshacheza filamu nne ndani ya miaka 11 na amefanikiwa kuingiza kiasi cha £38 milioni na kumzidi mwigizaji wa mwanzo aliyekuwa anacheza filamu hizo, Pierce Brosnan.