Kiongozi aliyeanzisha Wizara ya ‘Furaha na Utoshekaji kwa Wanandoa’ azua gumzo

Gavana wa jimbo moja kusini mwa Nigeria ameibua maswali na mijadala mizito nchini humo baada ya kuunda wizara mpya ya furaha na kutimizaji malengo.


Gavana Rochas Okorocha
Gavana huyo wa jimbo la Imo, Bw. Rochas Okorocha amejikuta akiambulia kejeli nchini Nigeria huku wananchi wengi wakionekana kumkosoa kwa kitendo cha kuanzisha Wizara hiyo.
Akizungumza na gazeti la Van Guard la nchini Nigeria, Okorocha amesema ameamua kuanzisha Wizara hiyo ili kuleta furaha kwa watu wanaijeria.
“Kwa bahati mbaya kwenye serikali yetu hakuna wizara wala idara yoyote inayoshughulikia masuala ya furaha ndio maana nimefanya hivyo hii sio kwa watu wa jimbo la IMO bali ni kwa wananchi wote. Kwani kila mtu ana malengo fulani katika maisha yake na ili ayafikie ni lazima awe na furaha ya nafsi, nadiriki kusema furaha ina gharama kubwa ingawaje watu wengine hujua hilo wakishaanza kupatwa na matatizo ya kiafya.”amesema Okorocho kwenye taarifa iliyonukuliwa na Van Guard.
Bwana Okorocha wiki chache zilizopita alishambuliwa vikali na wananchi wa Nigeria baada kuweka sanamu za kiongozi wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
Raia wengi Nigeria wamelaumu maamuzi hayo wengi wakihoji majukumu na umuhimu wa Wizara hiyo, na wengine wakidai kuwa ni mianya ya uvujaji wa fedha.
Tayari Gavana Okorocha ameshamchagua Kamishna wa Wizara hiyo kwa kumteua dada yake wa kuzaliwa tumbo moja, Ogechi Ololo kitendo ambacho kimeibua maswali ya upendeleo wa madaraka ndani ya utawala wa Rais wa nchi hiyo, Muhhamed Buhari.
Hata hivyo wakati Gavana Okorocha akimuapisha mdogo wake amesema kulikuwa na tatizo la uchapaji wizara hiyo inaitwa , Wizara ya Furaha na Utimizaji malengo na sio Furaha na Utoshekaji wanandoa’
Soma zaidi HAPA kuhusu mabadiliko ya wizara hiyo yaliyotolewa jana na Gavana wa jimbo la Imo.
Cheki baadhi ya maoni ya wadau mitandaoni.
Don't let Rochas Okorocha and his trademarks idiocy distract you from the things that really matter. Operatives of SARS are still roaming the streets, Yomi Shogunle is on a rampage, SARS reorganisation is a scam. 


Not only  ! We need to End alot of people in this country. E.G Rochas Okorocha
Rochas Okorocha appointed his Sister Ogechi Ololo (nee Okorocha) as Commissioner for Happiness and Couples' Fulfillment? Forget about the nepotism, that is now a regular in both Federal and State governments, but what is commissioner for happiness? Imo una Governor no well at all

Dear Rochas Okorocha,
Thank you for trying to distract us from the  campaign with your sisters appointment as 'Commissioner for Happiness'
May the God we serve visit you with heat rashes and small pox.
We will continue.  
 

735 likes